Visiwa vya vya
zanzibar nimevinakishia kwa Suratul-Raad aya ya 4 isemayo “ na katika
vipande vya ardhi vilivyokaribiana na kuna maabustani ndani yake ,kuna mizabibu
na mitende na mimea mengine inayotokana na shina moja na isiyotokana na shina moja yakinyweshelezwa (kumiminiwa ) na
maji ya aina moja ( INDIAN OCEAN) na tunaigawa matunda kutokana na utamu wake na
kwamba ndani ya mimea hii iliyotajwa
kuna ishara kwa wanaotia mambo akilini”
MDELLE
Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni chupa ya kahawa (
mdele) .Nimeinakishia kwa aya ya Suratul-ttur na mursalat
inayozungumzia vinywaji na vyakula isemayo “ watambiwa kuleni kunyweni kwa raha kabisa kwa yale ambayo mlioyatenda”
hii aya inashiria nini? Inasema" kila unachokila na unachokunywa ni akhalaq zako ni
tabia zako",ndo mana ALLAH alivowakataza
watu wasile ngurue anamaaana kuwa ana kitu ambacho kitakupelekea kutoka “HAYA”
Na kama mtu akikosa haya atakosa IMAN na kama mtu atakosa iman atakuwa hayupo katika
maadili na mlolongo wakisslamu au wakibinaadamu.
UPANGA
Ama taswira inayoonekana hapa ni upanga wa Sayyidna Ally bin abi Taalib ukifahamika kwa jina
maarufu ZULFIKAR ,lengo kuu sikushajihisha watu kupigana bali
nikiashiria roho iliyomo ndani ya ule upanga(uislamu) ,waliuweza kuushika
upanga maswahaba pale walivyoweza
kuvuta subra (religion tolorence) .Kwa hiyo sharti ya kuweza
upanga (dini kiislamu) huo ni kuwa na subra.Na ndo mana walikuwa ni wingi wa
subra mpaka wakamuuliza RASUUL “ ….. nusra ya ALLAH itakuja lini” RASSUUL akasema “ nusra ya ALLAH IKO KARIBU.
SAA YA KIZAMANI
Ama taswira
inavyoonekana hapa ni taswira ya Saa. Allah (s.w) anaizungumza saa katika
Suratul-ahzab aya ya 63, sivyo tunavooitumia leo
sisi ummat Muhammad( s.a.w ) .Tunaiona saa kwa kujikumbushia vikao tofauti vya
dunia kama kumuona rais au mtu yeyote kwa masuala ya dunia lakini ALLAH alvoitaja ndani ya QURAN kuwa inakumbusha
kuhusu mambo mingi
Tuikumbuke saa wa siku hakuna dawa itakayokufaa
Tuikumbuke saa wa siku ukayofumba jicho lako
Tuikumbuke saa wa siku utaingizwa ndani ya mwana wa ndani
Tuikumbuke saa wa siku utauliza masuala ndani ya kaburi
Tuikimbuke saa wa siku wa siku ambayo hakuna atakaezungumza
isipokuwa ALLAH
NI JUU YETU TUIJUE
SAA KWA MTAZAMO HUU SI KWA KUMBUKA MAMBO YA MPITO YA KIDUNIA
SUHFI ZA KALE
Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni SUHFI ZA KALE zikieleweka
kwa jina la kiengereza “scrolls” .Hizi ni karatasi ama suhfi zikitumika
kwa lengo la kueka ujumbe ama maandiko maalum kama baadhi yamitume walizitumia
suhfi kwa lengo hilo na kuwalingania umma wao.Nabbii Mussa na Ibraheem walikuwa katika mitume
walozotumia suhfi hizi katika kuweka ujumbe
kwa kuwalingania umma wa kiislamu.na ama aya nilizotumia kwa kunakishia
zinazungumzia katika Suratul Aalaa”hakika ni katika suhfi za mwanzo … suhfi Ibraheema na
Mussa….” Inaeleza hivo na ama aya ya pili katika Suratul- Mariam inasema “ na tunamtaka katika Quaran
Ibaheem kwamba hakika alikuwa ni katika
mitume wa kweli nan i nabii”……..” na tunamtaja ndani ya Quran Musaa yeye alikuwa ni katika mitume wenye ikhlas na ni mtume
na ni nabii.”nimeinakishia katika meza
pembezoni kutaja habari zao wa wakati
wao.
MSIKITI WA MADINA
BAIT-AMAAN
Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni BAIT-AMAAN ( MAKUMBUSHO) kutokana na sehemu yenyewe ni sehemu ya
kuweka kumbukumbu za nchi za taifa la ZANZIBAR ,kulingana na matukio ya
kihistoria za wanazuoni , mashekhe, na viongozi
mbali mbali,na aya niliyotumia kunakishia ni aya katika Suratul-Ankabut aya ya mwisho inayosema “ na wale ambayo
wanaofanya jihadi (ya aina yoyote) tutawaongoza katika njia (ya haki) zetu, na
kwamba ALLAH (S.W) yupo pamoja na wanaofanya haki”. Kwahivyo juu yetu
wazanzibari kutunza kumbukumbu za maimamu na wanazuoni wetu na viongozi wetu
tofauti ndani ya nchi nan je ya nchi za kiislamu ili zije kutunufaisha katika
vizazi vyetu vijavyo.
BAIT-ALJAIB
Ama kwa taswira inavyonekana ni BAIT- ALJAIB .Nimenakishia kwa Suratul-Yassin kuwa moyo wa Zanzibar ni
bait –aljaib kuwa ni Serekali ya Zaznibar ilikuwa ni hilo jengo ,shughulizote za serekali zilikuwa
zinafanyika tangu 1800-1970 ,nikilinganisha moyo wa Quran ni Yaasin.
Nimelingaanishakuwa baada ya viongozi wake walizingatia kwa kujitahidi kuweka
uislamu hai katika visiwani ZANZIBAR na aya zinamsifia Mtume (s.a.w) alikuwa ni kiongozi kupitia aya
tatu za mwanzo katika Suratul –Yaasin Yaasin…… na kwamba
Quran ni hakeem…….. kwamba Mtume alikuwa katika wenye kubeba na kuufikisha huo
ujumbe ……… juu ya kuongoz awatu katika njia ilionyooka …….. ambaye (kaifundisha
na )kaiteremsha mwenye nguvu na mwenye
kurehemu .’
MAUWA
Ama kwa taswira
inayoonekana hapa ni picha ya mauwa 3.Nimenakishia kwa
Suratul-Qasas inayosema “ na akasema mke wa firaauni huyu ni kitulizacho jicho
kwangu na mwako………”nimenakkishia kwa uwa au mauwa kwasababu inabeba sifa ya
uzuri kama alivobeba sifa Nabii Mussa ndio akasema maneno hayo,na uwa wewe
mwenyeo ukiliona unahisi au unafika kusema linakutuliza moyo ama jicho lako kwa
mujibu wa aya yenyewe na unakuwa unafarajika nalo kwa uzuri wake.
KARAFUU
Ama kwa taswira inavyonekana kwa picha inavvonekana ni KARAFUU
(CLOVE) kama ilivozoeleka kuwa karafuu ni dawa katika maradhi tofauti
inatumika katika dawa za meno , mafuta tofauti,kama ya kupaka miguu n.k.,
lakini tumesahau kuwa SHIFAA YA ALLAH inatibu hata maradhi ya uchumi,baada
ya kuzingatia na kuboreshana kuitunza karafuu ya Zanzibar ikaleta shufaa kubwa
katika uchumi wa zanziabar ,ikanaza kwa wakulima,familia,mitaa na hata mikoa ya zanizbar mpaka taifa zima la
Zanzibar na uongozi wake wote.Kwasababu
karafuu ni shifaa na shifaa huwa si ya mwili tu bali hata uchumi ukiwa na
maradhi basi huwa ni shifaa na ikaleta shifaa katika taifa la Zanzibar na
uongozi wote
MARFAA
Ama kwa taswira
inayoonekana hapa ni kwa sura ya marfa
ambao mara nyingi chombo hichi hutumika kwa masuala ya kusambaza
elimu,ndani ya madarsa ,vyuoni na sehemu nyengine maalum kwa ajili ya kupeleka
uislamu mbele na kutoa elimu za darja tofauti.Na ama aya nilizotumia kuchora
hii marfa ni” Mola wangu tuzidishie
elimu na turuzuku fahamu na utunufaishe tulichokifahamu ama tulojifunza”
kwahiyo juu yetu kujiombea dua hii kila siku ili ALLAH (S.W) atupe elimu na
aturuzuku fahamu na tuwe walimu wazuri na tuzae vipaji tofauti, na ama ya pili
niliyotumia ni “ utakasiko ni wako hatuna elimu isipokuwa uliotufunza na kwamba ni mwenye hekma na mwenye elimu” . hii ni kauli waliosema Malaika baada kutahayari kuwa ALLAH alivotaka
kumumba Binaadamu walisema kuwa wataleta ufisadi katika ardhi ,, bali ALLAH
aliwajib juwa mimi ninajua msioyajua, basi juu yetu watu wenye elimu kutokuwa
na kiburi mbele ALLAH kwani hapendi wenye tabia hio.
MSHUMAA
Ama taswira
inayoonekana hapa ni kwa picha ya MSHUMA
, aya niliyotumia nia katika Suratul- Ambiyaa aya ya 107
inayosema “ hatumpeleka MTUME isipokuwa awe rehma kwa ulimwengu mzima “
neon rahma linamaana nyingi kama muangaza ,rizki ,maghfira n.k.,na kwa
vile hii imekuja mfumo wa fasihi kuwa neon
kupeleka katika lugha ya kiarabu halikumtaja NENO Muhammad bali limesema “ tumekupeleka “ kwa mantiki ya
kuwa chochote chenye kumithilika angalau mithili ya muangaza kama mshumaa na
imethibiti kuwa ni rehma kwa ulimwengu wote na hakuna maskini wala tajiri
asietumia mshumaa huu
MIZANI
Ama picha saba inavyo onekana kwa taswira ya mizani .Na
kawaida ya mizani ina onesha uzito wa jambo au kitu katika moja ya
upande ama nime nakishia kwa Suratul- Tiyn inayosema “inakubidi vipi
muslim(muislamu wa kweli usiamini kwamba Allah(S.W) wamahakimu juu ya mahakimu
wote” kwa vile mizani ni chombo kina cho sisitiza uadilifu juu yetu Waislamu na
wasio kua waislamu kua na uadilifu katika kila jambo hata kama hatuna uwezo
tujitahid ili tuwe katika kupata rehema za Allah (S.W) wataala natukae kujua
juu ya kuhukumu kwetu mahkamani na
sehemu nyengine zote zenye kufanana na mahkamani watu wajue kwamba Allah (S.W) mmbora
wa kuhukumu kushinda wote . Na aya ya pili niliyo nakishia isemayo “ Hii ni
hiyo siku hamto zungumza kattu” ni kwamba hakuna mfale ,raisi wala raiya wake
wala wafuasiwa viongozi watakao kua na uwezo wakusema ispokua Allah (S.W) .
LOGO
Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni picha ya logo yangu
ambayo imeonekana katika kadi zangu za mualiko ,broshua na kadhalika. Lakini
aya nilizotumia ni kujiombea dua mimi na wazee wangu na ndugu zangu na waislamu
wote kwa ujumla .Na dua nilizotumia zinatuombea sote waislamu na khassa khasaa
ndugu zangu na wazee wangu kuwa “ YAA RABII TUGHUFURIE DHAMBI ZETU NA KWA WALE WOTE WALIOTANGULIA
WAKIWEMO NDUGU ZANGU KATIKA UISLLAMU KWA IMAN WALA USIWAJAALIE KIPANDE CHOCHOTE
CHA KIBRI KWA WALE WALIOAMINI . YAABII WEWE NI GHAFOOR NA WEWE NI RAHEEM” YAA
RABII TUPE KATIKA DUNIA HII YALIYO MAZURI NA TUPE KATIKA AKHERAA YALIYO MAZURI YOTE NA TUEPUSHE NA ADHABU YA
MOTO “ “ YAA RABII TUPE KATKA SISI KATIKA REHMA ZAKO NATUPE WEPESI KATIKA AMRI ZAKO JUU YAKUWEZA
KUTUONGOZA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA”.
JAMBIA
Ama kwa taswira inayoonekan hapa inalingana na taswira ya
upanga wa SAYYIDNA ALLIY BIN ABI TALLIB
ambayo maelezo yake yanalingana . Wako katika maswahaba waliulingania uislamu
kwa panga na wako kwa jambiia kwa wakati wa mtume na sio wakati wake.
ZAWADI
NGAO
Ama
kama picha taswira inavoonekana
kwa hapa ni taswira ya NGAO . Hadithi nyingi zimeelezwa kuwa ayatul kursiyyu ni kinga ya muislamu kwa maovu yote .Na ikiwa muislamu akiyamini basi ALLAH atamnusuru.
kwa hapa ni taswira ya NGAO . Hadithi nyingi zimeelezwa kuwa ayatul kursiyyu ni kinga ya muislamu kwa maovu yote .Na ikiwa muislamu akiyamini basi ALLAH atamnusuru.
Laweza kuja suala kuwa haya ni maneno na mie ni binaadamu , vipi yataninusuru?
ALLAHsaa. Allah (s.w) aliweka AHADI kuwa hakuna atakaeweza kubadilisha Quran yangu na ataihifadhi ,so kama alivowaachia watu wakabadilisha vitabu vitatu tauraat, injil, zabur bali QURAN ATAIHIFADHI DAIMA , kusema hivo kuwa anamaanisha kawekaanaizungumza saa katika kila herufiSuratul-ahzab sivyo tunavooitumia leo sisi ummat Muhammad( s.a.w ) .Tunaiona saa kwa kujikumbushia vikao tofauti vya dunia kama kumuona rais au mtu yeyote kwa masuala ya duania lakini ALLAH alvoitaja ndani ya Quran malaika kazi yake ni kuilinda QURAN TUKUFU na ndio maana unaposoma AYATUL-KURSIYYU wale malaika wanakuja na kuteremka kwa ajilia ya kulinda wewe na uwovu , huwa ni kama ngao kwako kwa kila baya au mbaya kama hadithi zinavosema.QURAN kuwa inakumbusha kuhusu mambo mingi
Utakua ALLAH (S.W) AMEWAPA WAISLAMU TEKNOLOJIA KUBWA KUSHINDA YAO WAO SASA WATU WANAOIPENDA DUNIA NA KUIPAMBA DUNIA NA HUWA WANAICHANA AKHERA YAO.Ni juu yetu waislam tuthamini kwa akile alichotupa RASSUUL (S.A.W) kuwa kina maana na sisi.Tuikumbuke saa wa siku hakuna dawa itakayokufaa
NGAO
Masha-Allah. Keep up the good work.
ReplyDeleteNi nzuri but nahisi ungeliulizia kisharia inafaa kufanya hivyo maana nahisi hizi ni aya ambazo ili zifikie kuwa haya maumbo unazichanganya vibaya hizi aya za allah. Nadhani umenielewa nini nakusudia. Ni hizi aya kuzichanganya kama ulivyofanya wewe jee inafaa
ReplyDeleteyap inafaaa kisharia na ushahidi upo
ReplyDeleteMashallah nice work Majid..
ReplyDelete