My Quranic Arts

CHEMCHEM (FOUNTAIN) 
Ama picha inayoonekana hapa ni kwa taswira ya chemchem(fountain) na aya  nilizotumia kunakishia ama kuchorea kupata picha hii ni inasema “tumejalia kila kinachotokana na maji kuwa kinakuwa hai” kuwa uhai wa hii chemchem ni kuwepo haya maji kutoka ujengaji wake mpaka ufanyaji  kazi wake  na aya ya pili niliyotumia kunakishia inasema “ na tuteremshie mteremsho wenye barka  nae ni mbora wakuteremsha mteremsho huo” kwa mantiki yakuwa  ALLAH (S.W)  kajalia kuwa mteremko wa mvua , wa kunywa maji, na huu huu wa chemchem ni mteremko  wenye barka mbele ya ALLAH (S.W)  kuwa maji yanateremka kuenda chini hata wanasayansi huita  ( under gravity) ALLAH kaita  “ munzalan” , kwahivyo maji ya mvua kushuka ama kuteremka mteremko usiokuwa wa aina hii itakuwa khasara na hapatokuwa ni penye maana ya mvua ,chemchem na mengine yenye mfanano kama huu. Kutokana ana aya hii ni mteremsho wenye  barka mbali na hivi sio wenye barka.PEMBA

UNGUJA 
Visiwa vya  vya zanzibar nimevinakishia kwa Suratul-Raad aya ya 4 isemayo “ na katika vipande vya ardhi vilivyokaribiana na kuna maabustani ndani yake ,kuna mizabibu na mitende na mimea mengine inayotokana na shina moja na isiyotokana  na shina moja yakinyweshelezwa (kumiminiwa ) na maji ya aina moja ( INDIAN OCEAN) na tunaigawa matunda kutokana na utamu wake na kwamba  ndani ya mimea hii iliyotajwa kuna ishara kwa wanaotia  mambo akilini”


MDELLE

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni chupa ya kahawa ( mdele) .Nimeinakishia  kwa aya ya Suratul-ttur na mursalat inayozungumzia vinywaji na vyakula isemayo “ watambiwa kuleni kunyweni  kwa raha kabisa kwa yale ambayo mlioyatenda” hii aya inashiria nini? Inasema" kila unachokila na unachokunywa ni akhalaq zako ni tabia zako",ndo mana ALLAH  alivowakataza watu wasile ngurue anamaaana kuwa ana kitu ambacho kitakupelekea kutoka “HAYA” Na kama mtu akikosa haya atakosa IMAN  na kama mtu atakosa iman atakuwa hayupo katika maadili na mlolongo wakisslamu au wakibinaadamu.

UPANGA
Ama taswira inayoonekana hapa ni upanga wa Sayyidna Ally bin abi Taalib ukifahamika kwa jina maarufu ZULFIKAR ,lengo kuu sikushajihisha watu kupigana bali nikiashiria roho iliyomo ndani ya ule upanga(uislamu) ,waliuweza kuushika upanga maswahaba  pale walivyoweza kuvuta subra (religion tolorence) .Kwa hiyo sharti ya kuweza upanga (dini kiislamu) huo ni kuwa na subra.Na ndo mana walikuwa ni wingi wa subra mpaka wakamuuliza RASUUL “ ….. nusra ya ALLAH itakuja lini”  RASSUUL akasema “ nusra ya ALLAH IKO KARIBU.

SAA YA KIZAMANI
   Ama taswira inavyoonekana hapa ni taswira ya Saa. Allah (s.w) anaizungumza saa katika Suratul-ahzab aya ya 63, sivyo tunavooitumia leo sisi ummat Muhammad( s.a.w ) .Tunaiona saa kwa kujikumbushia vikao tofauti vya dunia kama kumuona rais au mtu yeyote kwa masuala ya dunia lakini ALLAH  alvoitaja ndani ya QURAN kuwa inakumbusha kuhusu  mambo mingi

Tuikumbuke saa wa siku hakuna dawa itakayokufaa

Tuikumbuke saa wa siku ukayofumba jicho lako

Tuikumbuke saa wa siku utaingizwa ndani ya mwana wa ndani

Tuikumbuke saa wa siku utauliza masuala ndani ya kaburi

Tuikimbuke saa wa siku wa siku ambayo hakuna atakaezungumza isipokuwa ALLAH

NI JUU YETU  TUIJUE SAA KWA MTAZAMO HUU SI KWA KUMBUKA MAMBO YA MPITO YA KIDUNIASUHFI ZA KALE
Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni SUHFI ZA KALE zikieleweka kwa jina la kiengereza “scrolls .Hizi ni karatasi ama suhfi zikitumika kwa lengo la kueka ujumbe ama maandiko maalum kama baadhi yamitume walizitumia suhfi kwa lengo hilo na kuwalingania umma wao.Nabbii  Mussa na Ibraheem walikuwa katika mitume walozotumia suhfi hizi katika kuweka ujumbe  kwa kuwalingania umma wa kiislamu.na ama aya nilizotumia kwa kunakishia zinazungumzia katika Suratul Aalaa”hakika ni katika suhfi za mwanzo … suhfi  Ibraheema na  Mussa….” Inaeleza hivo na ama aya ya pili katika Suratul- Mariam  inasema “ na tunamtaka katika Quaran Ibaheem  kwamba hakika alikuwa ni katika mitume wa kweli nan i nabii”……..” na tunamtaja ndani ya Quran Musaa  yeye alikuwa ni  katika mitume wenye ikhlas na ni mtume na  ni nabii.”nimeinakishia katika meza pembezoni kutaja habari zao  wa wakati wao.

MSIKITI WA MADINA

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni taswira ya msikiti wa Madina wa MTUME (S.A.W) ambao unasifika kwa sifa kubwa ya ibada tofauti hata mahujaji na watu waumini tofauti huhudhuria hapo kwa ajili ya ibada.Nimeunakishai katika Suratul-Nnur aya ya 36 inayosema kwa mujibu wa sifa yake" na katika nyumba za ALLAH zinaleta wito kwa masail tofauti(adhana)kwa kumdhujuru na kutaja utajo wake na kupanda juu ndani yamsiiti huo , wanamsabihi ALLAH asubuhi na jioni" , na utakuta hio sehemu inatukuka kwa ibada tofauti namsikiti wa makka.


BAIT-AMAAN

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni  BAIT-AMAAN ( MAKUMBUSHO)  kutokana na sehemu yenyewe ni sehemu ya kuweka kumbukumbu za nchi za taifa la ZANZIBAR ,kulingana na matukio ya kihistoria za wanazuoni , mashekhe, na viongozi  mbali mbali,na aya niliyotumia kunakishia ni aya katika Suratul-Ankabut  aya ya mwisho inayosema “ na wale ambayo wanaofanya jihadi (ya aina yoyote) tutawaongoza katika njia (ya haki) zetu, na kwamba ALLAH (S.W) yupo pamoja na wanaofanya haki”. Kwahivyo juu yetu wazanzibari kutunza kumbukumbu za maimamu na wanazuoni wetu na viongozi wetu tofauti ndani ya nchi nan je ya nchi za kiislamu ili zije kutunufaisha katika vizazi vyetu vijavyo.


BAIT-ALJAIB
        Ama kwa taswira inavyonekana ni  BAIT- ALJAIB .Nimenakishia  kwa Suratul-Yassin kuwa moyo wa Zanzibar ni bait –aljaib kuwa ni Serekali ya Zaznibar ilikuwa ni hilo jengo  ,shughulizote za serekali zilikuwa zinafanyika tangu 1800-1970 ,nikilinganisha moyo wa Quran ni Yaasin. Nimelingaanishakuwa baada ya viongozi wake walizingatia kwa kujitahidi kuweka uislamu hai katika visiwani ZANZIBAR na aya zinamsifia  Mtume (s.a.w) alikuwa ni kiongozi kupitia aya tatu za mwanzo katika Suratul –Yaasin Yaasin…… na kwamba Quran ni hakeem…….. kwamba Mtume alikuwa katika wenye kubeba na kuufikisha huo ujumbe ……… juu ya kuongoz awatu katika njia ilionyooka …….. ambaye (kaifundisha na )kaiteremsha  mwenye nguvu na mwenye kurehemu .’

MAUWA

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni picha ya mauwa 3.Nimenakishia kwa Suratul-Qasas inayosema “ na akasema mke wa firaauni huyu ni kitulizacho jicho kwangu na mwako………”nimenakkishia kwa uwa au mauwa kwasababu inabeba sifa ya uzuri kama alivobeba sifa Nabii Mussa ndio akasema maneno hayo,na uwa wewe mwenyeo ukiliona unahisi au unafika kusema linakutuliza moyo ama jicho lako kwa mujibu wa aya yenyewe na unakuwa unafarajika nalo kwa uzuri wake.

KARAFUU


Ama kwa taswira inavyonekana kwa picha inavvonekana ni KARAFUU (CLOVE) kama ilivozoeleka kuwa karafuu ni dawa katika maradhi tofauti inatumika katika dawa za meno , mafuta tofauti,kama ya kupaka miguu n.k., lakini tumesahau kuwa   SHIFAA  YA ALLAH inatibu hata maradhi ya uchumi,baada ya kuzingatia na kuboreshana kuitunza karafuu ya Zanzibar ikaleta shufaa kubwa katika uchumi wa zanziabar ,ikanaza kwa wakulima,familia,mitaa na hata  mikoa ya zanizbar mpaka taifa zima la Zanzibar  na uongozi wake wote.Kwasababu karafuu ni shifaa na shifaa huwa si ya mwili tu bali hata uchumi ukiwa na maradhi basi huwa ni shifaa na ikaleta shifaa katika taifa la Zanzibar na uongozi wote


MARFAA

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni kwa sura ya  marfa ambao mara nyingi chombo hichi hutumika kwa masuala ya kusambaza elimu,ndani ya madarsa ,vyuoni na sehemu nyengine maalum kwa ajili ya kupeleka uislamu mbele na kutoa elimu za darja tofauti.Na ama aya nilizotumia kuchora hii marfa  ni” Mola wangu tuzidishie elimu na turuzuku fahamu na utunufaishe tulichokifahamu ama tulojifunza” kwahiyo juu yetu kujiombea dua hii kila siku ili ALLAH (S.W) atupe elimu na aturuzuku fahamu na tuwe walimu wazuri na tuzae vipaji tofauti, na ama ya pili niliyotumia ni “ utakasiko ni wako hatuna elimu isipokuwa uliotufunza  na kwamba ni mwenye hekma na mwenye  elimu” . hii ni kauli waliosema  Malaika baada kutahayari kuwa ALLAH alivotaka kumumba Binaadamu walisema kuwa wataleta ufisadi katika ardhi ,, bali ALLAH aliwajib juwa mimi ninajua msioyajua, basi juu yetu watu wenye elimu kutokuwa na kiburi mbele  ALLAH  kwani hapendi wenye tabia hio.


MSHUMAA

Ama taswira inayoonekana hapa ni kwa picha ya MSHUMA  , aya niliyotumia nia katika Suratul- Ambiyaa aya ya 107 inayosema “ hatumpeleka  MTUME  isipokuwa awe rehma kwa ulimwengu mzima “ neon rahma linamaana nyingi kama muangaza ,rizki ,maghfira n.k.,na kwa vile hii imekuja mfumo  wa fasihi kuwa neon kupeleka katika lugha ya kiarabu halikumtaja NENO Muhammad  bali limesema “ tumekupeleka “ kwa mantiki ya kuwa chochote chenye kumithilika angalau mithili ya muangaza kama mshumaa na imethibiti kuwa ni rehma kwa ulimwengu wote na hakuna maskini wala tajiri asietumia mshumaa huu

MIZANI


Ama picha saba inavyo onekana kwa taswira ya mizani .Na kawaida ya mizani ina onesha uzito wa jambo au kitu katika moja ya upande ama nime nakishia kwa Suratul- Tiyn inayosema “inakubidi vipi muslim(muislamu wa kweli usiamini kwamba Allah(S.W) wamahakimu juu ya mahakimu wote” kwa vile mizani ni chombo kina cho sisitiza uadilifu juu yetu Waislamu na wasio kua waislamu kua na uadilifu katika kila jambo hata kama hatuna uwezo tujitahid ili tuwe katika kupata rehema za Allah (S.W) wataala natukae kujua juu ya kuhukumu kwetu mahkamani  na sehemu nyengine zote zenye kufanana na mahkamani watu wajue kwamba Allah (S.W) mmbora wa kuhukumu kushinda wote . Na aya ya pili niliyo nakishia isemayo “ Hii ni hiyo siku hamto zungumza kattu” ni kwamba hakuna mfale ,raisi wala raiya wake wala wafuasiwa viongozi watakao kua na uwezo wakusema ispokua Allah (S.W) .

LOGO

Ama kwa taswira inayoonekana hapa ni picha ya logo yangu ambayo imeonekana katika kadi zangu za mualiko ,broshua na kadhalika. Lakini aya nilizotumia ni kujiombea dua mimi na wazee wangu na ndugu zangu na waislamu wote kwa ujumla .Na dua nilizotumia zinatuombea sote waislamu na khassa khasaa ndugu zangu na wazee wangu kuwa “ YAA RABII TUGHUFURIE  DHAMBI ZETU NA KWA WALE WOTE WALIOTANGULIA WAKIWEMO NDUGU ZANGU KATIKA UISLLAMU KWA IMAN WALA USIWAJAALIE KIPANDE CHOCHOTE CHA KIBRI KWA WALE WALIOAMINI . YAABII WEWE NI GHAFOOR NA WEWE NI RAHEEM” YAA RABII TUPE KATIKA DUNIA HII YALIYO MAZURI NA TUPE KATIKA AKHERAA  YALIYO MAZURI YOTE NA TUEPUSHE NA ADHABU YA MOTO “ “ YAA RABII TUPE KATKA SISI KATIKA REHMA ZAKO  NATUPE WEPESI KATIKA AMRI ZAKO JUU YAKUWEZA KUTUONGOZA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA”.

JAMBIA

Ama kwa taswira inayoonekan hapa inalingana na taswira ya upanga wa SAYYIDNA   ALLIY BIN ABI TALLIB ambayo maelezo yake yanalingana . Wako katika maswahaba waliulingania uislamu kwa panga na wako kwa jambiia kwa wakati wa mtume na sio wakati wake.


ZAWADI


Kama inavoonekana kwa taswira ya zawadi nimeinakishia kwa Suratul – Baqarah aya ya 197 kuwa peyaneni zawadi kwani ubora wa zawadi ni kumcha Allah (S.W), kuwa hata ukimpelekea swahib yako basin i wajib wako ama inafaa kumuusia  amche ALLAH ( S.W) ikawa zawadi ya pili badala ya kumpa zawadi moja tu iliyomo mule ndani


NGAO


Ama kama picha taswira inavoonekana
   kwa hapa ni taswira ya NGAO . Hadithi nyingi zimeelezwa kuwa ayatul kursiyyu ni kinga ya muislamu kwa maovu yote .Na ikiwa muislamu akiyamini basi ALLAH atamnusuru.

  Laweza kuja suala kuwa haya ni maneno na mie ni binaadamu , vipi yataninusuru?


  ALLAHsaa. Allah (s.w) aliweka AHADI kuwa hakuna atakaeweza kubadilisha Quran yangu na ataihifadhi ,so kama alivowaachia watu wakabadilisha vitabu vitatu tauraat, injil, zabur bali QURAN ATAIHIFADHI DAIMA , kusema hivo kuwa anamaanisha kawekaanaizungumza saa katika kila herufiSuratul-ahzab sivyo tunavooitumia leo sisi ummat Muhammad( s.a.w ) .Tunaiona saa kwa kujikumbushia vikao tofauti vya dunia kama kumuona rais au mtu yeyote kwa masuala ya duania lakini ALLAH alvoitaja ndani ya Quran malaika kazi yake ni kuilinda QURAN TUKUFU na ndio maana unaposoma AYATUL-KURSIYYU wale malaika wanakuja na kuteremka kwa ajilia ya kulinda wewe na uwovu , huwa ni kama ngao kwako kwa kila baya au mbaya kama hadithi zinavosema.QURAN kuwa inakumbusha kuhusu mambo mingiUtakua ALLAH (S.W) AMEWAPA WAISLAMU TEKNOLOJIA KUBWA KUSHINDA YAO WAO SASA WATU WANAOIPENDA DUNIA NA KUIPAMBA DUNIA NA HUWA WANAICHANA AKHERA YAO.Ni juu yetu waislam tuthamini kwa akile alichotupa RASSUUL (S.A.W) kuwa kina maana na sisi.Tuikumbuke saa wa siku hakuna dawa itakayokufaa

                                                                          NGAO


4 comments:

  1. Masha-Allah. Keep up the good work.

    ReplyDelete
  2. Ni nzuri but nahisi ungeliulizia kisharia inafaa kufanya hivyo maana nahisi hizi ni aya ambazo ili zifikie kuwa haya maumbo unazichanganya vibaya hizi aya za allah. Nadhani umenielewa nini nakusudia. Ni hizi aya kuzichanganya kama ulivyofanya wewe jee inafaa

    ReplyDelete
  3. yap inafaaa kisharia na ushahidi upo

    ReplyDelete